As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Tuesday, January 1, 2019

TUMIA MAJI SAFI

Katika nchi fulani si rahisi kupata maji safi ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Hata hivyo, kutopatikana kwa maji safi kunaweza kuwa tatizo popote ulimwenguni ikiwa chanzo kikuu cha maji safi ya kunywa kitachafuliwa kutokana na mafuriko, kimbunga, kuharibika kwa bomba, au jambo lingine lolote. Ikiwa chanzo cha maji si safi au hakijatunzwa vizuri, maji yanaweza kusababisha magonjwa yanayotokana na vimelea, kama vile kipindupindu, ugonjwa hatari wa kuharisha, homa ya matumbo, mchochota wa ini, na magonjwa mengine. Maji yasiyo salama ni moja ya chanzo cha ugonjwa wa kuharisha kwa visa vya watu bilioni 1.7 hivi kila mwaka.


Kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kupunguza au kuzuia kuanza kwa ugonjwa

Mara nyingi mtu huambukizwa ugonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa maji au kula chakula kilicho na viini kutoka kwa watu walioambukizwa. Unaweza kuchukua hatua gani ili kujilinda hata baada ya kupatwa na ugonjwa au maambukizo mengine yanayotokana na maji yasiyo salama?

    Hakikisha kwamba maji unayokunywa, kutia ndani maji unayotumia kusafisha meno, kugandisha barafu, kusafisha chakula na vyombo, au kupikia, yanatoka kwenye chanzo salama, kama vile bomba la umma, lenye maji yaliyowekwa dawa ili kuua viini au maji ya chupa yanayotengenezwa na kampuni inayoaminika.

    Ikiwa maji ya bomba unayotumia si safi, chemsha maji kabla ya kutumia au weka dawa ya kuua viini.

    Unapotumia kemikali au dawa za kuua viini katika maji, kama vile klorini au dawa za kusafisha maji, fuata maelekezo ya watengenezaji.

    Tumia mashine ya kuchujia maji iliyo bora ikiwa inapatikana na ikiwa unaweza kununua.

    Ikiwa hakuna dawa za kuua viini katika maji, tumia dawa ya kuondoa madoa, weka matone mawili katika lita moja ya maji, changanya vizuri, na kisha acha maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kuyatumia.

    Sikuzote hifadhi maji safi katika vyombo vilivyo safi na ufunike ili kuzuia yasichafuliwe kwa njia yoyote.

    Hakikisha kwamba vyombo vinavyotumiwa kuchota maji kama vile kikombe ni safi.

    Mikono yako inapaswa kuwa safi unapotumia au unapogusa vyombo vinavyotumiwa kutunza maji, na usitumbukize mikono yako au vidole katika maji ya kunywa.

No comments:

Post a Comment