Mtu anahitaji chakula chenye lishe bora ili awe na afya nzuri. Huenda ukahitaji kuchunguza matumizi yako ya chumvi, vyakula vyenye mafuta, sukari, na unapaswa kujua kiasi cha chakula unachokula. Unapokula tumia pia matunda, mboga, na uwe na kawaida ya kula vyakula vya aina mbalimbali. Soma maelezo yaliyo katika pakiti ya bidhaa ili uweze kununua vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa kama vile mkate, nafaka yenyewe, tambi, au mchele. Vyakula hivi vina virutubisho na nyuzinyuzi kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka zilizokobolewa. Ili kupata protini, kula kiasi kidogo cha nyama ya ng’ombe na kuku, na ikiwezekana jitahidi kula samaki mara kadhaa kwa juma. Katika nchi fulani ni rahisi kupata vyakula vyenye protini kutoka kwenye mboga.
Ukiwa na zoea la kula vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta yaliyoganda, unaweza kunenepa kupita kiasi. Ili kuepuka hilo, kunywa maji badala ya vinywaji vyenye sukari. Kula matunda zaidi badala ya vyakula vyenye sukari. Punguza kiasi cha vyakula vyenye mafuta unachotumia kama vile soseji, nyama, siagi, keki, jibini, na biskuti. Na badala ya kupika kwa kutumia mafuta yaliyoganda, lingekuwa jambo linalofaa kutumia mafuta yanayofaa mwili.
Kutumia chumvi au sodiamu kupita kiasi unapokula, kunaweza kuongeza shinikizo la damu kwa kiwango kisichofaa kwa mwili. Ikiwa una tatizo hilo, soma maelezo yaliyo katika pakiti ya chakula ili ujue jinsi ya kudhibiti matumizi yako ya sodiamu. Badala ya kutumia chumvi, tumia vikolezo na viungo ili kufanya chakula chako kiwe na ladha.
Kiasi unachokula kina umuhimu sawa na chakula unachokula. Hivyo, usiendelee kula chakula ikiwa tayari umeshiba, hata kama unafurahia kula chakula hicho.
Jambo lingine kuhusu lishe ni hatari ya kula chakula kisichofaa. Chakula chochote kisipotayarishwa na kutunzwa vizuri kinaweza kukuletea madhara. Kila mwaka, mtu 1 kati ya 6 nchini Marekani anaugua kutokana na kula chakula kisichofaa. Wengi wao hupona kwa muda mfupi, hata hivyo kuna wachache wanaokufa. Unaweza kufanya nini ili kuepuka hatari hiyo?
• Kwa kuwa mboga hukuzwa katika udongo ambao huenda umewekwa mbolea, safisha vizuri mboga kabla ya kupika.
Safisha kwa maji moto yenye sabuni, mikono yako, ubao unaotumia kukatia mboga, vyombo, na kaunta za jikoni kabla ya kuanza kuandaa chakula.
Ili kuepuka kuchafua chakula safi, epuka kukiweka katika sahani au chombo chochote kisichosafishwa kilichokuwa kimetumiwa kuweka mayai mabichi, kuku, nyama, au samaki.
Pika chakula vizuri na tunza mara moja katika friji vyakula vyovyote vinavyoweza kuharibika ikiwa unapanga kula baadaye.
Tupa chakula chochote kinachoweza kuharibika kilichoachwa kwa zaidi ya saa mbili au moja katika hali ya hewa inayozidi nyuzi joto 32.
Tuesday, January 1, 2019
KULA CHAKULA KINACHOFAA
Tags
# AFYA CLICK
About afya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
AFYA CLICK
Labels:
AFYA CLICK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment