As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Monday, October 28, 2019

TAMBUA UGONJWA WA INI

Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu, hufanya kazi zaidi ya 500 ; moja ya kazi ni kuchuja na kuondoa sumu kutoka kwenye damu.
Kutokana na sababu mbalimbali kama pombe iliyopita kiasi, sumu kwenye damu au maambukizi; ini hupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. Hii hali huitwa HOMA YA INI au HEPATITIS.
Katika maeneo yetu, bara la Afrika maambukizi ya virusi wa Homa ya ini ndio sababu kuu ya shida kwenye ini. Virusi vya Homa ya ini vipo vya aina 5 (A,B,C,D,E).
Aina mbili za virusi (B na C ) ndio sababu kuu za ugonjwa wa homa ya ini na husambaa kupitia damu na majimaji ya mwili.
Homa ya ini ni sawa janga linaloua kimya kimya kulingana na takwimu za vifo za dunia inakadiriwa Kirusi cha homa ya ini aina ya B pekee huua watu 600,000 hivi kila mwaka.
Kwa wastani zaidi ya watu bilioni mbili, yaani, asilimia 33 hivi ya watu wote ulimwenguni, wameambukizwa virusi vya HBV, na wengi wao hupona baada ya miezi michache. Watu milioni 350 hivi huendelea kuwa na virusi hivyo mwilini, wengi huishi bila dalili na kuendelea kuambukiza watu wengine

NAMNA GANI UNAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI (B NA C)…….?

Virusi vya homa ya ini B na C husambaa kupitia damu, shahawa au maji maji mengine ya mwili.
Virusi hivi vina uwezo wa kusambaa na kuambukiza mtu mara 100 zaidi ya virusi vya UKIMWI.
Njia hizi husambaza virusi hivi vya homa ya ini..:
  1. Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
    Mama aliye na maambukizi ya Hepatitis B kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua, iwapo hamna juhudi za kitiba za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza mtoto.
  2. Kufanya mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini
  3. Kuchangia vifaa vyenye ncha Kali kama sindano hasa kwa watumia madawa ya kulevya au wachora tattoo, miswaki
  4. Kuongezewa damu ambayo ina maambukizi ya homa ya ini.

Virusi vya homa ya ini vinaweza ishi nje ya mwili kwa muda mrefu…

Tafiti zinaonyesha virusi vya homa ya ini vinaweza ishi nje ya mwili hadi kwa muda wa siku 7, bado vikiwa na uwezo wa kuambukiza mtu. Tafiti zimeonyesha hata iliyokauka huwa na uwezo wa kuambukiza virusi hivi

NANI YUPO KATIKA HATARI ZAIDI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HOMA YA INI?

° Watoto wachanga waliozaliwa na mama aliye na maambukizi ya virusi vya homa ya ini
° Watu wanaofanya biashara ya ngono
°Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao
°Watu wanaojidunga dawa za kulevya
° Mtu mwenye mpenzi ambaye anaishi na maambukizi ya virusi vya homa ya ini
° Wafanyakazi wa sekta ya Afya
° Watu wa familia wenye ndugu anayeishi na maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini
°Wagonjwa wa figo wanaotumia huduma za kusafisha damu (dialysis)

No comments:

Post a Comment