As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Tuesday, January 1, 2019

Njia za Kuboresha Afya Yako


NANI anapenda kuwa mgonjwa? Hakuna anayependa, kwa kuwa ugonjwa ni kikwazo na ni chanzo cha gharama. Unapokuwa mgonjwa, huhisi tu vibaya bali pia huenda ukashindwa kwenda kazini au shuleni, kutafuta pesa, au kuitunza familia yako. Huenda hata ukahitaji mtu fulani akutunze, na huenda ukahitaji kulipia gharama za dawa na matibabu.

Kuna msemo usemao “Kinga ni bora kuliko tiba.” Baadhi ya magonjwa hayaepukiki. Hata hivyo, bado kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kupunguza au hata kuzuia kuanza kwa ugonjwa. Fikiria mambo matano unayoweza kufanya ili kuwa na afya bora.
Kulingana na Kliniki ya Mayo, “njia moja bora zaidi ya kujikinga na ugonjwa na kuepuka kueneza ugonjwa” ni kunawa mikono. Ni rahisi kupata homa au mafua kama utagusa pua au macho yako huku mikono yako ikiwa na viini. Njia bora ya kujilinda na maambukizi ni kunawa mikono yako kwa ukawaida. Kudumisha usafi kunaweza pia kuepusha kuenea kwa magonjwa hatari kama vile, nimonia na magonjwa ya kuharisha, ambayo kila mwaka husababisha vifo vya watoto zaidi ya milioni mbili, walio chini ya umri wa miaka mitano. Hata kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola, kunaweza kupunguzwa kwa kuwa na kawaida ya kunawa mikono.

Kuna pindi ambazo ni muhimu kunawa mikono ili kulinda afya yetu na ya wengine. Unapaswa kunawa mikono:

    Baada ya kutoka chooni.

    Baada ya kumbadilisha nepi mtoto au kumsaidia kutumia choo.

    Kabla na baada ya kutibu jeraha au kidonda.

    Kabla na baada ya kumtembelea mgonjwa.

    Kabla ya kutayarisha, kuhudumia, au kula chakula.

    Baada ya kupiga chafya, kukohoa, au kupenga kamasi.

    Baada ya kumgusa mnyama au kinyesi cha mnyama.

    Baada ya kutupa takataka.

Usifikiri kwamba kunawa mikono yako kikamili ni jambo lisilo muhimu. Uchunguzi umeonyesha kwamba asilimia kubwa ya wale wanaotumia vyoo vya umma hawanawi mikono yao vizuri au hawanawi kabisa. Unapaswa kunawa mikono yako jinsi gani?

    Lowesha mikono yako katika maji safi ya bomba na kisha utumie sabuni.

    Sugua mikono yako pamoja ili kupata povu, bila kusahau kusafisha kucha, vidole, pande zote za mkono, na katikati mwa vidole vyako.

    Endelea kusugua kwa sekunde 20 hivi.

    Safisha mikono yako katika maji safi yanayotiririka.

    Kausha mikono yako kwa kutumia kitambaa safi au karatasi ya kukaushia mikono.

Ni rahisi kufanya mambo hayo, na kufanya hivyo kunaweza kuzuia ugonjwa na kuokoa uhai.

No comments:

Post a Comment