As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Tuesday, December 18, 2018

KANUNI YA MSINGI YA KUPUNGUZA UZITO

Kanuni Ya Msingi
Kila unapokula chakula kinatakiwa kutumika na mwili, kama ikitokea umekula chakula kingi na mwili ukatumia kidogo maana yake chakula kingine kinabadilishwa na kuhifadhiwa mwilini kama mafuta ambayo ndio yanayokufanya kuwa na uzito kupita kiasi.

Na kama chakula kinachofika kwenye damu ni kidogo kuliko mahitaji ya mwili, mwili utadhoofu na uzito mdogo kupita kiasi utaonekana.

Kwa hiyo, ili kuwa na uzito sahihi kanuni hii lazima izingatiwe.


Chakula kinachoingia =Chakula kinachotumika


UONGO KUHUSU KUPUNGUZA UZITO

Watu wengi hudanganyika eti kufanya mazoezi na kupunguza kula kunasaidia mtu kupunguza uzito hii sio kweli, nitaeleza kwa nini..

Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kuhamasisha kazi za mwili (metabolism) kufanya kazi barabara.
MF. Kama umekula sana ukafanya mazoezi maana yake unahamasisha kile chakula pamoja na kutumika kitengeneza nguvu kwa ajili ya mazoezi pia kusaidia shughuli zingine za mwili kufanya kazi vema, ikiwemo kubadili hicho chakula kilichozidi kuwa mafuta na uzito kuongezeka.


Sikatai, ni kweli mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia kupunguza uzito lakini ufanisi wake ni pungufu ya 20% katika mchakato mzima.

Wala huna haja ya kujinyima chakula ili kupunguza uzito…


Fanya haya machache wewe mwenyewe utanipatia majibu kwamba ulipata uzito ulikuwa unataka..

Tumia wanga isiyochakatwa/ kukobolewa katika asili yake mfano Mchele wa brown, viazi, ngano isiyokobolewa, nafaka zisizokobolewa, n.k hivi vina nyuzinyuzi nyingi kwa hiyo huujaza mfumo wa chakula bila kutoa calories/nguvu nyingi sana kuliko hitaji la mwili.
Kula matunda kama yalivyo (si katika hali ya juisi) pia yananyuzinyuzi na huleta matokeo kama hapo juu.
Ongeza mbogamboga mbichi au zilizopitishwa kwenye mvuke (isiyopikwa sana) kadhalika kuna nyuzi nyuzi kwa kazi ileile.
Usisahau vyakula jamii ya Karanga na mbegu zote itakusaidia sana kupata protin salama kwa afya yako na pia kuleta hali ya kutosheka na Chakula.

No comments:

Post a Comment