As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Tuesday, December 18, 2018

Njia Kwa Vitendo- Punguza Uzito

Uzito mkubwa au mdogo kupita kiasi ni hatari kiafya.
Kiwango cha uzito kuwa mdogo au mkubwa ninachokizungumzia hapa kinaweza kupimwa kwa namna 2 ili kuwa na uhakika.

Njia ya kwanza unaweza kupima kwa kutumia BMI (Body Mass Index) ambapo unachukua uzito wako (kg) unagawanya kwa kipeo cha pili cha urefu wako katika kipeo cha pili cha mita (m)².

Majibu yako utakayopata yalinganishe na haya

BMI MAONI
Chini ya 18.5 Uzito mdogo kupita kiasi
18.5-24.9 Kawaida
25-29.9 Uzito mkubwa kupita kiasi
30+ Kiriba tumbo

Aina hii ya upimaji ina changamoto kwa baadhi ya watu mfano wanaofanya mazoezi sana misuli inakuwa mikubwa sana na BMI zinaonekana kuwa juu lakini hawana kiriba tumbo. Kwa wazee na watu wembamba sana wanaweza kuonekana wanauzito mdogo kupita kiasi kama ukitumia BMI lakini si kweli.


Ili kuhakikisha kuna njia nyingine mtu anaweza kujipima kujua yupo upande gani.

Hapa tunatumia WHR (Waist to Hip Ratio). Unapima kwa kutumia futi kamba juu tumboni juu ya kidogo ya kitovu (sehemu nyembamba kuliko zote tumboni), na pia unapima kiunoni/hips (sehemu Nene kuliko zote kiunoni). Halafu gawanya ile ya tumboni na kiunoni. Kisha linganisha na hizi.


Wanawake ikizidi 0.8 ni hatari na kwa wanaume ikizidi 0.95 ni hatari.


Hii tunaifanya kwa sababu watu ambao wanamaumbo ya tofaa (apple) kwa maana ya kwamba mafuta mengi yamelundamana tumboni kuliko sehemu zingine wanahatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari, kiharusi, saratani, matatizo ya mifupa n.k ukilinganisha na watu wenye maumbo ya pear kwa maana mafuta anayo mengi lakini yamesambaa karibu mwili wote.

No comments:

Post a Comment