Antibiotiki ni dawa za kupambana na maambukizi kutokana na bakteria. Hazisaidii dhidi ya maambukizi ya virusi kama vile tetekuwanga, surua ya rubella, mafua, au homa ya kawaida. Siyo kila antibiotiki inaweza kupambana na maambukizi ya bakteria. Dawa za antibiotiki zenye muundo wa kemikali unaofanana huchukuliwa kuwa katika familia moja. Ni muhimu kuwa na ufahamu juu ya familia za antibiotiki kwa sababu kuu 2:
Dawa za antibiotiki kutoka katika familia moja mara nyingi hutibu matatizo yanayofanana.
Kama una mzio kutokana na dawa moja ya antibiotiki kutoka katika familia moja, utapata mzio pia kutokana na dawa za antibiotiki zingine kutoka familia hiyo. Hii inamaanisha kwamba unatakiwa kutumia dawa kutoka katika familia nyingine ya antibiotiki.
Dawa ya antibiotiki lazima itumike “kwa dozi kamilifu.” Kukatisha dozi bila kukamilisha siku zote za matibabu, hata kama utakuwa umepata nafuu, kunaweza kusababisha maambukizi kurudia katika muundo ambao utakuwa mgumu zaidi kutibika.
Ampisilini na amoksilini
Ampisilini na amoksilini ni familia ya penisilini yenye tiba pana, maana yake ni kwamba huua aina nyingi za bakteria kuliko dawa zingine katika kundi hili la penisilini. Dawa hizi 2 mara nyingi ni mbadala wa nyingine. Pale ambapo ampisilini imependekezwa katika kitabu hiki, amoksilini inaweza kutumika katika nafasi yake kwa kuzingatia dozi sahihi.
Ampisilini na amoksilini ni dawa salama sana na ni msaada mkubwa kwa watoto wachanga na watoto wadogo. Inapotolewa pamoja na dawa zingine, ampisilini ni tiba muhimu kwa vidonda vya tumbo na kwa ajili ya maambukizi ya ngozi ya fumbatio(peritonitisi).
Madhara ya pembeni
Dawa hizi 2, lakini hasa ampisilini, huwa na tabia ya kusababisha kichefuchefu na kuharisha. Epuka kutoa dawa hizi kwa watoto ambao tayari wanaharisha - kama unaweza wapatie dawa aina nyingine ya antibiotiki.
Madhara mengine ya kawaida ya pembeni ni upele. Uvimbevimbe, mithili ya malengelenge, unaowowasha ambao huja na kutoweka ndani ya saa chache huenda ni dalili ya mzio kutokana na penisilini. Simamisha utoaji wa dawa hiyo mara moja na usimpe mtoto huyu penisilini tena. Matukio ya usoni yanaweza kuwa mabaya zaidi na hata kutishia maisha. Kwa baadhi ya matatizo, erithiromaisini inaweza kutumika. Upele ulioenea tambarare ukifanana kama wa surua, na kawaida kuanza wiki moja baada ya kuanza kutumia dawa na ambao huchukua siku kadhaa kutoweka, mara nyingi siyo dalili ya mzio. Lakini haiwezekani kujua kwa uhakika iwapo upele huo unatokana na mzio au la, hivyo ni bora kusimamisha dawa.
Tuesday, March 5, 2019
ANTIBIOTIC VIUA VIJISUMU
Tags
# AFYA CLICK
About afya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
AFYA CLICK
Labels:
AFYA CLICK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment