As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Tuesday, January 1, 2019

LALA VYA KUTOSHA

KIASI kinachohitajika cha usingizi kinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Watoto wengi wachanga hulala saa 16 hadi 18 kwa siku, watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi mitatu hulala saa 14 na wale wenye umri wa miaka mitatu hadi minne hulala saa 11 au 12 hivi. Watoto walio na umri wa kutosha kwenda shule kwa ujumla wanahitaji kulala kwa saa 10, vijana kwa saa 9 au 10, na watu wazima kwa saa 7 hadi 8.

Kulala vya kutosha hakupaswi kuonwa kuwa ni uamuzi tu wa mtu. Kulingana na wataalamu, kulala vya kutosha ni muhimu kwa ajili ya:

    Ukuzi na maendeleo ya watoto na vijana.

    Kujifunza na kukumbuka habari mpya.

    Kudumisha usawaziko unaofaa wa homoni zinazosaidia kumeng’enya chakula na uzito wa mwili.

    Kudumisha moyo wenye afya nzuri.

    Kuzuia magonjwa.

Kutolala vya kutosha kumetajwa kuwa chanzo cha kunenepa kupita kiasi, kushuka moyo, ugonjwa wa moyo, kisukari na chanzo cha aksidenti mbaya. Bila shaka, mambo hayo yanatufanya tuwe na sababu nzuri za kuhakikisha kwamba tunalala vya kutosha.

Hivyo, ufanye nini ukigundua kwamba haulali vya kutosha?

    Lala na amka muda uleule kila siku.

    Jitahidi kufanya chumba chako cha kulala kiwe na utulivu, chenye giza, cha kustarehesha, na kisiwe na joto au baridi sana.

    Usitazame Televisheni au kutumia kifaa cha kielektroniki unapokuwa kitandani.

    Jitahidi kadiri uwezavyo kufanya kitanda chako kiwe chenye kustarehesha.

    Epuka kula vyakula vizito, kafeini, na kileo kabla ya kulala.

    Ikiwa hata baada ya kufuata mapendekezo hayo bado unakosa usingizi au una magonjwa mengine yanayohusiana na usingizi kama vile kulala au kusinzia kupita kiasi mchana au kupumua kwa shida unapolala, huenda ikafaa zaidi kumwona daktari.

No comments:

Post a Comment