Watu milioni 49 hufa kila mwaka ulimwenguni pote. Asilimia 75 hivi ya vifo hivi hutokea mapema mno, kisababishi kikihusiana na mazingira na mtindo-maisha mbaya, kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Fikiria baadhi ya vielelezo:
▪ Kansa huua watu milioni tano kila mwaka. Sehemu kubwa ya hii, laripoti WHO, “hasa ni kwa sababu ya ongezeko kubwa katika uvutaji sigareti katika miaka 30 iliyopita.”
▪ Maradhi ya kuhara, yanayoua zaidi ya watoto milioni tatu kila mwaka, mara nyingi husababishwa na chakula na maji yaliyotiwa uchafu, na vilevile ukosefu wa usafi ufaao.
▪ Kifua kikuu, muuaji wa watu milioni tatu kila mwaka, husitawi katika mazingira ya umaskini na yenye kusongamana kwa watu, hasa mahali ambako hakuna usafi.
▪ Maambukizo ya mfumo wa upumuaji, hasa mchochota wa pafu, huua watoto milioni tatu na nusu wenye umri wa chini ya miaka mitano kila mwaka. Wengi ni wakaaji wa majijini ambao wako katika hatari ya viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa.
Kando na hatari hizi ziletazo kifo, kila mwaka watu bilioni mbili na nusu—karibu nusu ya idadi ya watu ulimwenguni—hupatwa na magonjwa ambayo hutokana na ukosefu wa maji ya kutosha au yasiyo safi na ukosefu wa usafi. Kwa kuongezea, WHO inahusianisha mahangaiko ya wakati huu kama vile, mvua ya asidi, tabaka la ozoni lililopungua, na kuongezeka kwa joto duniani na afya yenye kuzorota ya wengi. Kwa ujumla, ikaonelea ripoti ya WHO, zaidi ya watu bilioni mbili huishi katika mazingira yenye kutisha uhai au yenye kutisha afya.
Dakt. Hiroshi Nakajima, mkurugenzi-mkuu wa WHO, aonya hivi: “Tusipotenda sasa, tatizo la Dunia na wakazi wayo litakuwa baya sana, kukiwa na mazingira ambayo hayawezi kutegemeza tena.”
Biblia yaahidi kwamba kutakuwa na wakati ambapo “hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa.” (Isaya 33:24) Hilo litatimizwa, si na jitihada za mwanadamu, bali na Ufalme wa Mungu, ambao utakomesha magonjwa na visababishi vyayo.—Ufunuo 21:3, 4.
Thursday, January 10, 2019
Tags
# AFYA CLICK
About afya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
AFYA CLICK
Labels:
AFYA CLICK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment