As we all know that Healthy matters,lets follow the readings for longevity of our lives now and then for sustainable healthy affairs

Monday, December 17, 2018

VYAKULA VYA KUNENEPESHA

kumekua na tafiti nyingi zinzoonyesha vyakula vipi vinanenepesha watu zaidi duniani, japokua kila chakula kinategemea na kiasi unachokula lakini baadhi ya vyakula hunenepesha sana vinapoliwa na ni hatari kwa afya kwani huleta magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo na saratani ambayo yanaongoza kuua watu wengi zaidi duniani kila mwaka. kama wewe ni mnene unataka kupungua, kama wewe ni mwembamba unataka kubaki hivyohivyo basi kaa mbali na hivi.


Chipsi; hiki ni chakula kinacholiwa sana na watu duniani, kwani ni rahisi kuandaa na kukiuza na ukiwachunguza walaji wa chakula hichi  hua wana vitambi sana  au ni wanene..chips husababisha mazoea yaani addiction ambayo humfanya mlaji atamani kuzila kila siku na kunenepa zaidi kwani ukizila husikii kushiba na kula nyingi zaidi.

Vyakula vya kukaangwa; vyakula vyote vya kukaangwa kama maandazi, vitumbua, chapati,sambusa, soseji,  nyama na mikaango yote unayofahamu hua na mafuta mengi ambayo mafuta hayo huingia mwilini na kumfanya muhusika awe mnene sana.

No comments:

Post a Comment