Majani na maua ya Moringa yanavirutubisho vingi kama vitamin A (mara tatu zaidi ya karoti), vitamin C (mara tatu zaidi ya ile ya machungwa), calcium
(mara 140 zaidi ya ile inayopatikana katika maziwa ya ngombe) na potasiamu. Umetumika katika kusaidia udhibiti wa matatanisho yanayoletwa na ugonjwa wa ukimwi.
Inakostawi
Nchi zote za joto tropics na subtropics, sana sana katika sehemu za pwani, hupendelea mwinuko wa kati ya 0-500m. Hustawi sana sehemu za Ukanda wa
Bahari ya Hindi. Asili ya mmea wa Moringa ni wenyeji wa sehemu ya Sub Himalaya kaskazini magharibi mwa nchi ya India.
Uhifadhi wa majani ya moringa Majani ya Moringa hukaushwa na kusagwa ili kutengeneza unga ambao huongezwa kwenye chakula kama viazi vilivyosetwa na uji wa mahindi ama mtama ili kuongeza ubora wake.
Mapishi mbalimbali ya Mlonge
Majani ya mlonge na maharagwe
VIAMBA UPISHI
Majani ya mlonge 2 vikombe
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu saumu 3-4 punje
Kitunguu maji 1 kikubwa
Chumvi 1⁄2 kijiko cha chai.
Mafuta ya maji 2 vijiko vya kulia chakula
Tui la nazi 1⁄2 kikombe cha chai
Maharage 1 Kikombe
Nyama/samaki/kuku 1 kikombe cha vipande
vilivyokatwakatwa ili viwe vidogo
HATUA ZA MAPISHI
1. Chemsha maharage na kuku /nyama ya ngombe/ samaki mpaka iive.
2. Osha majani ya moringa vizuri, ondoa sehemu zisizohitajika na ukatakate.
3. Ambua, osha na ukatakate kitunguu maji na ukaange hadi kilainike.
4. Ambua, osha na uponde kitunguu saumu na uongeze kwenye kitunguuu maji.
5. Osha na ukatakate nyanya, ongeza kwenye mchanganyiko na uendelee kukaanga.
6. Ongeza majani ya moringa kwenye mchanganyiko,koroga na uendelee kukaanga.
7. Ongeza chumvi na upike hadi mboga zote ziive vizuri.
Chakula hiki cha majani kinaweza kuliwa pamoja na ugali, wali, na vyakula vinginevyo.
Mlonge na Matembele
VIAMBA UPISHI
Majani ya Mlonge 2 Vikombe
Matembele 2 Fungu
Mafuta ya kupikia 3 Vijiko vya kulia
vilivyosagwa 1 Kijiko cha chai
Kitunguu maji 1
Vitunguu saumu 3-4 punje
Nyanya 1
Karoti ndogo 1
Tui la nazi kikombe cha chai
Chumvi,kijiko cha chai.
HATUA ZA MAPISHI
1. Osha Moringa na Matembele vizuri huku ukitoa sehemu zisizo hitajika.
2. Tayarisha tui la nazi na upashe moto kwenye sufuria tofauti.
3. Ambua kitunguu maji, vitunguu saumu na karoti na uoshe pamoja na nyanya.
4. Katakata kitunguu, nyanya na karoti na uponde vitunguu saumu.
5. Pasha mafuta moto kwenye sufuria na ukaange kitunguu maji hadi kilainike.
6. Ongeza karoti na nyanya, koroga hadi mchanganyiko uwe laini. Ongeza chumvi na kitunguu saumu na ukoroge.
7. Ongeza tui moto la nazi na ukoroge hadi kufikia kuishia tui.
Mboga hii yaweza kuliwa na ugali, mihogo, wali na vyakula vinginevyo.
No comments:
Post a Comment